VPN na Proxy

VPN & PROXY ni nini?

VPN ni kifupi cha Virtual Private Network. Ni encrypted tunnel yaani njia ya kuficha utambulisho halisi wa kifaa au mahali kati ya vifaa viwili ambayo inakuwezesha kuingia kwenye kila website na huduma nyinginezo za mtandaoni privately na securely.
READ MORE →
Picha za Ubunifu

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI UNAFANYA UCHAGUZI WA PICHA KATIKA DESIGNING.

Ukiwa kama designer kuna mambo ya msingi unapaswa kuyafahamu wakati wa kuchagua picha ili uwe imara katika kutengeneza maudhui yako. Wengi katika wale wanaoanza kujifunza huwa hawazingatii suala la uchaguzi bora wa picha...
READ MORE →
Misingi ya Design

MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA KAZI ZA DESIGNING

Ukiwa kama designer kuna mambo ya msingi unapaswa kuyafahamu ili uwe imara katika kutengeneza maudhui yako. Wengi katika wale wanaoanza kujifunza huwa hawazingatii misingi ya designing hivyo hujikuta wanaishia njiani katika kazi zao.
READ MORE →
Picha PNG

WEBSITE 5 KWAAJILI YA KUDOWNLOAD PNG IMAGE

Miongoni mwa jambo ambalo linalochosha na kupoteza muda kwa designer wengi hasa kwa wale wanoanza ni kuondoa background katika picha. Kwa kawaida ili kutatua changamoto hii hutumia website au programu za nje...
READ MORE →

VPN & PROXY ni nini?

VPN na Proxy

VPN

VPN ni kifupi cha Virtual Private Network. Ni encrypted tunnel yaani njia ya kuficha utambulisho halisi wa kifaa au mahali kati ya vifaa viwili ambayo inakuwezesha kuingia kwenye kila website na huduma nyinginezo za mtandaoni privately na securely.

Hii ni teknolojia inayotumika kuunda muunganisho salama na wa faragha kati ya kifaa chako (kama simu au kompyuta) na mtandao, hasa unapotumia intaneti.

VPN hufanya nini?

  1. Kuficha utambulisho halisi wa kifaa : VPN inaficha anwani yako ya IP (IP address) ili shughuli zako za mtandaoni zisiweze kufuatiliwa kwa urahisi na watoa huduma za intaneti, wavamizi, au hata serikali.
  2. Inaongeza Usalama: Inaficha data zako hada pale unapojiunga na public network kama Wi-Fi za bure na kufanya kuwa ngumu wadukuzi kufikia taarifa zako.
  3. Inakupa uwezo wa kufikia mitandao au maudhui yaliyozuiwa katika nchi husika: Unaweza kufikia tovuti au huduma zilizozuiwa katika eneo lako kwa kuonekana kana kwamba unatoka nchi nyingine.

Jinsi Inavyofanya Kazi:

VPN hukuelekeza trafiki yako ya intaneti kupitia seva iliyoko mahali pengine duniani. Seva hiyo inakupa anwani mpya ya IP, ikificha eneo lako la kweli na kufanya encryption ya data zako.

Mifano ya VPN:

  • AvastVPN
  • ProtonVPN
  • Baadhi ya VPN za bure zinaweza kuwa na hatari za usalama au kushiriki data yako.
  • Matumizi ya muda mrefu ya VPN yanaharibu afya ya battery ya kifaa chako hasa simu
  • Ikiwa unahitaji VPN, chagua huduma inayotambulika na inayoaminika, na epuka zile za bure zisizo na sifa nzuri.

PROXY

Ni server au kompyuta inayotumika kama kituo cha kati kati ya vifaa vyako (simu, kompyuta) na mtandao wa internet. Tunapoitumia, huenda kwenye tovuti kwa niaba yako.

Aina za Proxy:

  1. HTTP Proxy: Hutumika kwa tajiri za wavuti pekee. Inasaidia kuvinjari mitandao.
  2. SOCKS Proxy: Inasaidia programu nyinginezo kama downloader za torrent na michuano.
  3. Transparent Proxy: Hutumiwa na wafanyabiashara kwa kulinda mtandao wao bila kubadilisha mipangilio ya vifaa vya watumiaji.

Faida za Proxy:

  • Inakuwezesha kufungua tovuti zilizozuiwa katika eneo lako.
  • Inaweza kuongeza kasi ya upakiaji wa tovuti kwa kuhifadhi nakala (caching).
  • Hutumika na makampuni kudhibiti matumizi ya wafanyikazi kwenye mitandao.

Hasara za Proxy:

  • Hailindi/ficha (encrypt) data yako - Unaweza kuonekana na mwenye server ya proxy.
  • Haifanyi kazi kwenye programu zote - inalenga kivinjari au programu fulani tu.
  • Proxy za bure zaweza kuwa na hatari - wengine hukusimulia na kuuza data yako.

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI UNAFANYA UCHAGUZI WA PICHA KATIKA DESIGNING.

Uchaguzi wa picha

Ukiwa kama designer kuna mambo ya msingi unapaswa kuyafahamu wakati wa kuchagua picha ili uwe imara katika kutengeneza maudhui yako.

Wengi katika wale wanaoanza kujifunza huwa hawazingatii suala la uchaguzi bora wa picha hivyo hujikuta wanatoa kazi zisizo na ubora.

Pia kutokuzingatia uchaguzi sahihi wa picha unaweza kupelekea watu kuacha kufuatilia kazi zako.

HAYA NI MAMBO MANNE UNAYOPASWA KUYAZINGATIA :

1. HATI MILIKI YA PICHA (copyright ©️)

>Unapochagua picha hakikisha picha hiyo haina hati miliki au kama inayo basi ni ruhusa kwa wengine kutumia, unaweza kujikuta matatizoni kutokana na kutumia picha ya mtu kinyume na ruhusa yake.

2. PICHA IZINGATIE MAADILI.

>Unapofanya uchaguzi wa picha hakikisha inazingatia maadili ya jamii kwa ujumla hii itasaidia kufikisha ujumbe kwa haraka pia husaidia katika kutengeneza kazi nzuri na za kuvutia

3. UHUSIANO KATI YA PICHA NA UJUMBE ULIOPO.

>Hili ni jambo la msingi sana katika designing kwasababu unapo fanya kazi fulani kisha ukaweka picha ambayo inaendana na ujumbe hufanya watu kuelewa kwa haraka kinyume chake huwafanya watu kufikilia na pengine kutoelewa umemaanisha nini.

4. UBORA WA PICHA(quality)

>Hiki nacho ni kipengele matata sana ambacho unapaswa kuzingatia. Ubora wa picha hufanya kazi kuwa angavu na ya kuvutia zaidi. Hivyo unapochagua picha hakikisha ina quality na resolution ya kutosha.

Ili kupata matokeo mazuri ya kazi zako, unaweza tembelea tovuti hizi ili kupata picha bora na free kutumia


KUMBUKA WEBSITE HIZO KUNA PICHA NYINGINE ZINAUZWA, BROWSE KISTAARABU BILA KUVUNJA SHERIA.

MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA KAZI ZA DESIGNING

Misingi ya Design

Ukiwa kama designer kuna mambo ya msingi unapaswa kuyafahamu ili uwe imara katika kutengeneza maudhui yako. Wengi katika wale wanaoanza kujifunza huwa hawazingatii misingi ya designing hivyo hujikuta wanaishia njiani katika kazi zao. Pia kutokuzingatia misingi hupelekea kufanya kazi zilizo chini ya ubora ukilinganisha na wengine.

HAYA NI MAMBO MATANO UNAYOPASWA KUYAZINGATIA :

1. PRINCIPAL OF DESIGN

Huu ndio msingi wa ubunifu ambao designer anapaswa kuzingatia. Msingi huu unahusisha matumizi sahihi ya rangi, mistari, nafasi na vitu vingine kabla ya kuanza kazi yako.

2. UCHAGUZI WA SOFTWARE & PROGRAM

Baadhi ya kuamua ni kitu gani unafanya, wapaswa kuchagua ni program gani utaenda kutumia katika kazi yako. Uchaguzi usio sahihi hupelekea matokeo tofauti na ulivyotarajia.

3. KUWA KARIBU NA WATU (WANAO FANYA KAZI KAMA ZAKO AU WAZOEFU KATIKA MASOKO)

Ili uweze kupata soko mapema, unatakiwa kuweka ushirikiano bora kati yako na watu walio juu yako ili panapotokea uhitaji wa mfanyakazi iwe rahisi kupatikana.

4. KUCHAGUA ENEO UTAKALO HUSIKA NALO

Kwa upande huu, designer hupaswi kuhusika na maeneo mengi kwa wakati mmoja ukiwa unaanza. Unapaswa uchague ni sehemu ipi sahihi uwe una deal nayo.

Mfano, photo editing, video editing au photography.

5. KUCHAGUA PORTFOLIO

Ili uweze kutoa kazi bora ni vema uanze na kulinganisha kazi yako na wengine wamefanya nini. Pia kubali kujitolea pale inapohitajika ili kukuza uwezo wa kudisign vilevile huongeza nafasi ya kupata ajira.

Nahisi umejifunza kitu, hivyo wewe kaamam designer fanya uchaguzi sahihi kabla ya kuanza kazi ya kuandaa maudhui.

WEBSITE 5 KWAAJILI YA KUDOWNLOAD PNG IMAGE

Picha bila background

Miongoni mwa jambo ambalo linalochosha na kupoteza muda kwa designer wengi hasa kwa wale wanoanza ni kuondoa background katika picha. Kwa kawaida ili kutatua changamoto hii hutumia website au programu za nje ili kuondoa background za picha.

Website pekee na nzuri inayotumika kuondoa background ya picha ni Remove bg unaweza kuingia hapa ili kutumia website hii https://www.remove.bg/

Hapa nimekuwekea website 5 bora ambazo unaweza kudownload picha bila background kwa urahisi zaidi.

  1. https://www.pngwing.com/
  2. https://www.pngtree.com/
  3. https://freepng.com/
  4. https://www.cleanpng.com/
  5. https://www.stickpng.com/